Kufuatia hali ya uvunjwaji wa haki za binadamu inayoendelea Tarafa ya Ngorongoro Wilayani Ngorongoro ambapo jamii ya wafugaji wa Kimaasai wameeleza kunyimwa haki zao za binadamu ikiwemo haki ya kupiga kura, asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikifuatilia jambo hilo zimetoa tamko la pamoja ambapo pamoja na mambo mengi limemshauri Rais Samia kufika eneo hilo aweze kujionea hali halisi pamoja na kuzungumza na wananchi.
Kadhalika kwa tume huru ya taifa ya uchaguzi, asasi zimeishauri iweze kuwarejeshea haki yao ya kuweza kuchagua na kuchaguliwa wakazi hao, sawasawa na sheria yza uchaguzi inavyoelekeza. Unaweza kusoma tamko hili kwa mapana yake kwa kubofya na kuipakua hapa.
Je unafahamu Mamlaka ya Uhifadhi ya Ngorongoro ilianzishwa mwaka 1959? Unajua ilikuwaje? Tazama video hii fupi uelewe mchakato mzima na mahitaji ya wananchi.