Salamu za pole na pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

SALAMU ZA POLE NA PONGEZI KWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN KUTOKA KWA WATETEZI WA HAKI NA ASASI ZA KIRAIA TANZANIA

Utangulizi

Wadau wa Sekta ya Asasi za Kiraia/Watetezi wa Haki za Binadamu tunapenda kutoa salamu za pole kwa Rais wetu, Mhe Rais Samia Suluhu kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Aidha, kwa pamoja tumeendelea kuungana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja, viongozi wengine wa serikali na watanzania wote kwa ujumla katika kuomboleza kifo cha Hayati Rais Magufuli. Wakati huo huo tunapenda kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Samia Suluhu kwa kupata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mchango wa Hayati Rais Magufuli katika Maendeleo

Wadau wa Sekta ya Asasi za Kiraia kwa ujumla tutamkumbuka Hayati Rais Magufuli kwa jitihada kubwa alizozifanya katika kuleta maendeleo, kupiga vita rushwa, na ufisadi, kuboresha miundo mbinu, kuboresha huduma za jamii, kuweka nidhamu ya utumishi wa umma nk. Tunatambua kuwa tangu mwaka 1995 alipochaguliwa kuwa Mbunge na baadae kuteuliwa kuwa Naibu Waziri, Waziri katika Wizara tofauti na baadae katika nafasi ya Rais, Hayati Rais Magufuli alikua mstari wa mbele katika kupinga rushwa na kuleta uwajibikaji katika idara za umma. Aidha Hayati Mh. Rais Magufuli alijitahidi kwa kiasi kikubwa kupigana vita dhidi ya umasikini na kuboresha miundo mbinu.

Tunatambua kuwa, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kulikua na kilio kikubwa cha wadau wa Asasi za Kiraia kuhusu mambo kadhaa ikiwemo kukosekana kwa uadilifu katika sekta ya umma, utawala wa sheria, katiba mpya, haki za binadamu, umaskini miongoni mwa jamii, changamoto katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, miundombinu na nishati.

Hayati Rais Magufuli alijitahidi sana kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hizi pamoja na kwamba zipo changamoto ambazo zilikuwa zinaendelea kufanyiwa kazi hadi umauti una mkuta. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali ikiwemo Ilani za Uchaguzi ya Asasi za Kiraia, yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu yaliyofanyika au kukamilika katika kipindi cha uongozi wake katika kukuza uchumi wa kitaifa.

(i)Kuendelea kuboresha utoaji na upatikanaji wa elimu kwa watoto. Utoaji wa elimu burekatika ngazi ya Elimumsingi ni hatua ya kupongezwa.

(ii)Kuongezeka kwa vituo vya afya, zahanati na hospitali kutoka 7,014 mwaka 2015 hadi8,446 mwaka 2020;

(iii)Kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutoleahuduma za afya kutoka asilimia 42 ya mahitaji mwaka 2015 hadi asilimia 94.5 mwaka2020;

(iv)Kukua kwa wastani wa pato la mwananchi kutoka shilingi 1,968,965 mwaka 2015 hadishilingi 2,458,496 mwaka 2018, na Pato la Taifa limeongezeka kwa wastani wa asilimia6.9 kwa mwaka.

(v)Kuboresha miundo mbinu ikiwemo miundombinu ya nishati kama vile umeme wa mtoRufiji, barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari. Haya yamefanyika kwa lengo lakurahisisha biashara na shughuli nyingine za kiuchumi kufanyika kwa urahisi na haraka.

(vi)Kuimarisha biashara kwa wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga, mama lishe) kwakuwaongezea unafuu wa kulipa ushuru wa Shilingi elfu 20 kila mwaka. Hali hii imechangiapia kurasimisha biashara hizi na kuongeza usalama wao ukilinganisha na hapo awaliwalipokuwa hawatambuliki na kunyanyasika sana.

(vii)Kufufua shirika la ndege la serikali (ATCL) kwa kununua ndege mpya kwa fedhataslimu. Hii ni hatua muhimu ambayo itatanua wigo kwa Watanzania kufanya biashara njena ndani ya nchi pamoja na kupanua sekta ya utalii nchini.

(viii)Kudhibiti mianya mingi ya wizi na utoroshwaji wa mali na rasilimali za taifa kamavile madini. Jambo hili limepelekea ongezeko la pato la ndani la taifa. Kwa mfano katikakipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2018/2019 (Julai – Novemba), makusanyoya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) yalifikia TZS 7.37 trlioni sawa na 88.9%ya makadirio ya TZS 8.30 trilioni katika kipindi hicho. Mapato yameendelea kukua mwakahadi mwaka kutokana na hatua stahiki zilizochukuliwa.

(ix)Kuongezeka kwa mapato yasiyo ya kodi – kutokana na kuimarishwa kwa ufuatiliajikwenye taasisi, mashirika na kampuni kulikoiwezesha serikali kupata michango na gawiostahiki kutoka kwenye uwekezaji wake.

(x)Kuimarika kwa matumizi ya technolojia katika ukusanyaji wa maduhuli kwenye wizara naidara zinazojitegemea kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato uitwao‘Government Electronic Payment Gateway’ (GePG) ambapo kati ya Julai 2017 hadiNovemba 2018, jumla ya Taasisi za Serikali 325 zinatumia mfumo huu kukusanyamaduhuli.

(xi)Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, kumekua na uongezeko la upatikanaji wa umemekutoka megawati (MW) 1,308 mwaka 2015 hadi megawati (MW) 1,602.32 mwaka 2020.Pia, usambazaji wa umeme vijijini umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 16.4mwaka 2015 hadi asilimia 67.1 mwaka 2020;

(xii)Kuimarisha juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, watotona wazee. Kutunga Sheria ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017 ilikua ni moja ya hatuakubwa kuhakikisha Serikali, Asasi za Kiraia na wadau mbalimbali wa haki za binadamuwanachangia katika kulinda na kutetea haki za binadamu.

(xiii)Uwepo wa utayari miongoni mwa wizara na idara mbalimbali za serikali kukutanana wadau wa Sekta ya AZAKI na kushirikiana nao kupunguza changamoto mbalimbali.Moja ya mikutano muhimu ni mkutano wa Januari 2021 uliokutanisha wadau wa AZAKIna Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambao uliibua mambo mengi ya kufanyiwa kazi. Mikutano ya kila mwaka ya Wakurugenzi wa Azaki ambapo wageni rasmi wamekuwa ni Mawaziri. Mikutano mbalimbali ya Azaki kufunguliwa na Viongozi wa Serikali nk.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu yatakayokumbukwa na wadau wa sekta ya Asasi za Kiraia nchini. Haya mambo aliyoyatekeleza Hayati Rais Magufuli yanahitaji kusimamiwa na kulindwa kwa umakini ili tusirudi tulipotoka. AZAKI tupo tayari kusaidiana na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza mazuri aliyosimamia Hayati Rais Magufuli. Kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Hayati Mhe. John Pombe Magufuli mahali pema peponi, Amina. Amemaliza kazi yake nzuri na ameatuchia sisi viongozi wenzake jukumu la kuyaendeleza.

Pongezi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan

Kufuatia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sisi wadau wa sekta ya Asasi za Kiraia tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Tuna Imani kubwa naye kwa utendaji kazi uliotukuka katika kipindi chote cha uongozi wake katika nafasi mbalimbali alizowahi kushika huko nyuma.

Itakumbukwa kuwa Mh. Rais Samia amekua mdau mkubwa wa sekta ya Asasi za Kiraia. Kabla ya kuingia kwenye siasa aliwahi kufanya kazi kwenye shirika la Association of Non-Governmental Organizations in Zanzibar (ANGOZA) pamoja na World Vision. Na baada ya kuingia katika nafasi za juu serikalini, mara kadhaa amekua mstari wa mbele kushiriki katika makongamano na mikutano mbalimbali ya Asasi za Kiraia na taasisi za kiserikali. Haya yote ni baadhi tu ya mambo yanayoendelea kutupa imani kubwa katika nafasi yake mpya kama Rais wetu na kwamba yeye ni mmoja wa viongozi wanaoijua vyema sekta hii ya Asasi za Kiraia.

Mnamo mwaka 2014 wakati wa mchakato wa kuandaa mapendekezo ya Katiba Mpya, Mhe. Rais Samia, akiwa Naibu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba alikua mstari wa mbele kuongoza majadiliano kati ya wananchi, wabunge wa Bunge la Katiba na wadau mbalimbali ili tuweze kupata Katiba bora ambapo mara kadhaa alishiriki mikutano mbalimbali ikiwemo ile iliyoandaliwa na wadau wa sekta ya Asasi za Kiraia.

Katika nafasi mbalimbali alizoshika Mhe. Rais Samia amekua pia mstari wa mbele kufanya kazi na wadau wa Asasi za Kiraia katika kuhakikisha mambo mbalimbali muhimu kwa jamii yanatekelezwa. Miongoni mwa maeneo muhimu aliyosimamia moja kwa moja ni pamoja na uboreshaji wa vituo vya afya na huduma ya afya, huduma ya maji (maarufu kama kampeni ya ‘kumtua mama ndoo’), kuboresha hali ya lishe kwa wakina mama wajawazito, watoto chini ya umri wa miaka mitano, vijana balehe, na wazee, na kuzindua mradi wa kutokomeza unyanyasaji wa wanawake na watoto masokoni. Pia amekua amekua akipambania kumuinua mwanamke kiuchumi pamoja na kuwa mlezi wa mabaraza ya kumuinua mwanamke kiuchumi.

Mwaka 2016, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe Ban Ki Moon alitangaza kuanzishwa kwa Jopo Kuu la Masuala ya Uwezeshwaji Wanawake Kiuchumi lilikuwa na jukumu la kuhamasisha hatua madhubuti za kuchukua katika kuleta usawa wa kijinsia, kutoa mapendekezo mahsusi ya utekelezaji wa malengo endevelu na hasa lengo namba 5 (kufikia usawa wa kijinsia; kuwawezesha wasichana na watoto) na lengo namba 8 (kuinua mustakabali wa kukuza uchumi na kuhakikisha ajira stahiki za kudumu). Aidha, Katibu Mkuu Mhe Ban Ki Moon alimteua Mhe Rais Samia akiwa

Makamu wa Rais kuwa Mjumbe wa Jopo Kuu la Viongozi wa Dunia kama Mwakilishi wa Nchi za Afrika hivyo Mhe Rais wetu, Mhe Rais Samia anaouelewa mpana sana wa masuala haya ambayo ndio kilio cha watoto, vijana na wanawake nchini.

Si hivyo tu. Mhe. Rais Samia ameshiriki katika makongamano mengi yaliyoandaliwa na Asasi za Kiraia kwa lengo la kujadili na kuboresha upatikanaji wa haki za makundi mbalimbali katika jamii kama vile haki za Wanawake na watoto. Katika nafasi mbalimbali alizoshika na hata katika nafasi yake ya Makamu wa Rais, amekua akishiriki katika makongamano mbalimbali, mfano makongamano ya wanawake na makundi mengine katika jamii.

Miongoni mwa mikutano iliyoandaliwa na AZAKI aliyopata kuhudhuria ni pamoja na Ushiriki wake wa karibuni kabisa mnamo Tarehe 8 Machi 2021, aliposhiriki katika Maandhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Mwanamke na Uongozi, na mkutano wa Mwanamke na Uongozi ulioandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) Machi 4, 2021. Mikutano mingine aliyohudhuria ni pamoja na ifuatayo.Uzinduzi wa Mtandao wa Wanawake Viongozi Bara la Africa mwaka 2020 (African Women Leaders Network-AWLN), Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka 2019 (Mtandao wa Wanawake na Katiba), Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini mwaka 2018 (Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania-TAWLA), Tamasha la 14 la Mtandao wa Kijinsia mwaka 2017 (TGNP), Maadhimisho ya Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania mwaka 2017 (THRDC), na Mkutano wa Watetezi wa Haki za Binadamu na Wabunge wa Bunge la Katiba mwaka 2014 (THRDC); na mikutano mingine.

Katika kushiriki mikutano ya AZAKI na kutoa ushirikiano kwenye kazi mbalimbali zinazoandaliwa na Asasi za Kiraia tunapata tumaini na nguvu kubwa ya kuimarisha utoaji huduma mbalimbali kwa jamii kupitia Asasi za Kiraia. Yafuatayo ni baadhi ya maeneo ya muhimu ambayo sisi Wadau wa sekta ya Asasi za Kiraia tunatarajia kuendelea kuboresha na kufanya kazi karibu zaidi na serikali ili kuhakikisha tunachangia katika mafanikio ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan:

(i) Kuendelea kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi kwa fedha zinazotumika katika miradi mbalimbali. Katika taarifa iliyotolewa na Asasi za Kiraia katika wiki ya Asasi za Kiraia Novemba 7 mwaka 2019, mashirika 16 yaliyofanyiwa utafiti yalionyesha yameingiza nchini shilingi bilioni 236 katika kipindi cha miaka mitatu tu (2016-2018) kwa ajili ya kutelekeza miradi mbalimbali nchini.

(ii) Kuboresha utendaji kazi wa Asasi za Kiraia na hivyo kuongeza tija katika utoaji wa huduma mbalimbali. Kwa mfano sisi wadau wa Asasi za Kiraia tutaendelea kusaidia katika kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za afya, elimu, maji na kadhalika.

(iii) Kuongeza miradi ya kibunifu na yenye tija kwa jamii na makundi mbalimbali kama vijana, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto na wazee.

(iv) Kuongeza uwezo wa kifikra na kiuchumi miongoni mwa wanajamii kupitia elimu na miradi mbalimbali ya kujenga uwezo itakayofanywa na wadau wa Asasi za Kiraia

(v) Kuchangia ongezeko la utawala bora katika taasisi za kiserikali kutokana na ufuatiliaji utakaoendelea kufanywa na Asasi za Kiraia na wadau mbalimbali wa utawala bora na haki za binadamu.

(vi) Kuchangia kutokomeza umaskini nchini kupitia miradi mbalimbali ya AZAKI.

(vii) Kushirikiana na serikali kutoa huduma kwa maeneo mbalimbali

(viii) Kuweka mikakati na serikali ya namna ya kutoa ajira kwa maelfu ya vijana Tanzania.

(ix) Kulinda Katiba, haki za binadamu na utawala bora

(x) Kutoa msaada wa kisheria kwa wasiokuwa na uwezo wa kuweka wakili

(xi) Kuendelea kuwa walipa kodi wazuri hapa nchini

(xii) Kufanya kazi zetu kwa uwazi na kwa weledi na kufuata miongozo ya serikali

(xiii) Kuishauri serikali katika mambo ya msingi yanayohusu usimamizi wa sekta ya AZAKI hapa nchini ikiwemo kuweka mazingira wezeshi ili sekta ya Asasi za Kiraia kukua na kustawi kama ambavyo Ilani ya CCM 2020-2025 ilivyoahidi

(xiv) Kumshauri Mhe Rais Pamoja na serikali kuendelea kusimamia utumishi wa umma kwa ukakamavu mkubwa kwa mujibu wa taratibu na misingi iliyopo ya kisheria.

(xv) Kuendelea kuishauri maboresho ya sheria mbalimbali kandamizi ikiwemo namna bora ya kuimarisha utawala bora

(xvi) Kuendelea kuvishauri Vyama vya Siasa kuweka utaratibu wa kupata na kutambua uwakilishi Bungeni wa Asasi za Kiraia (ikijumuisha mashirika ambayo sio ya kiserikali – NGOs) kama ambavyo Chama Cha Mapinduzi kilivyofanya na kuishauri Serikali kuwepo utaratibu wa kisheria wa kuitambua nafasi hiyo

(xvii) Kuendelea kuishauri serikali na wadau mbalimbali kuhusu kuboresha usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi.

(xviii) Kushauri viongozi, wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mambo muhimu yatakayoweza kuboresha Amani ya taifa letu kwa mujibu wa Katiba na Sheri za nchi yetu.

Ni imani yetu kuwa kutokana na kazi kubwa aliyofanya Mh. Rais Samia katika nafasi mbalimbali alizoshika, ataendelea kutumia uzoefu wake na kwa kushirikiana na viongozi wengine walio chini yake katika kuhakikisha kuwa taifa letu linaendelea katika mwelekeo mzuri wa kimaendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sambamba na hayo, ni matumaini yetu kuwa kadiri ambavyo ratiba yake itaruhusu, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan atatupa fursa ya sisi kama wadau wa Asasi za Kiraia kukutana nae ili kupata dira na mahitaji yake ya namna bora ya kuendeleza na kuimarisha mashirikiano kati ya Asasi za Kiraia na idara mbalimbali za serikali.

Hongera Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Mungu akulinde na akuongoze.

Mungu Ibariki Tanzania.

Imetolewa leo tarehe 29 March, 2021

Na Asasi za Kiraia Tanzania zilizorodheshwa hapa chini

1. ACT – MARA DIOCESE – MUGUMU SAFE HOUSE

2. ACTION AID

3. ACTION FOR CHANGE

4. ACTION FOR RURAL WOMEN EMPOWERMENT

5. ACTIONS FOR DEMOCRACY AND LOCAL GOVERNANCE (ADLG)

6. AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM

7. AGRI THAMANI FOUNDATION

8. AHADI FORUM TANZANIA (AFTA)

9. ALPHA AND OMEGA RECONCILIATION AND PEACE BUILDING (AREPEB)

10. AMANI GIRLS HOME

11. ARUSHA NON GOVERNMENTAL ORGANISATION NETWORK (ANGONET)

12. ASSOCIATION (TAMA)

13. ASSOCIATION FOR NON GOVERNMENTAL ORGANISATION ZANZIBAR (ANGOZA)

14. ASSOCIATION OF RARE BLOOD DONOR (ARBD)

15. AVIWATA

16. BASE FOR EDUCATION DISSEMINATION

17. BASE FOR EDUCATION DISSEMINATION (BED)

18. BETTER LIFE

19. BIHARAMULO COMMUNITY FM RADIO (BCFM)

20. BIHARAMULO NGOS NETWORK FORUM

21. BIHARAMULO ORIGINATING SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT ASSOCIATION (BOSEDA)

22. BIHARAMULO SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT ASSOCIATION (BISEDEA)

23. BUSSINESS AND HUMAN RIGHTS TANZANIA

24. CENTRE AGAINST GENDER BASED VIOLANCE (CAGBV)

25. CENTRE FOR WIDOWS & CHILDREN ASSISTANCE (CWCA )

26. CENTRE OF YOUTH DIALOGUE (CYD)

27. CESOPE

28. CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAENDELEO ZANZIBAR (WAHAMAZA)

29. CHIFU KIMWELI FOOTBALL CLUB

30. CHILD WATCH

31. CHILDREN DIGNITY FORUM

32. CHRISTIAN EDUCATION AND DEVELOPMENT ORGANIZATION (CEDO)

33. CIVIC AND LEGAL AID ORGANIZATION

34. CIVIC SOCIAL PROTECTION FOUNDATION (CSP)

35. COMMUNITY DEVELOPMENT INITIATIVES SUPPORT ORGANIZATION( COSIDO)

36. COMMUNITY FOR EDUCATORS AND LEGAL ASSISTANCE

37. COMMUNITY RESEARCH AND DEVELOPMENT SERVICES (CORDS)

38. COMMUNITY SUPPORT INITIATIVES –TANZANIA (COSITA)

39. CRISIS RESOLVING CENTRE

40. CRISIS RESOLVING CENTRE (CRC)

41. C-SEMA

42. DEVELOPMENT FOR ACCOUNTABILITY FOR TANZANIANS

43. DIGNITY KWANZA COMMUNITY SOLUTIONS

44. DOOR OF HOPE TO WOMEN AND YOUTH IN TANZANIA

45. DUNGONET (NGO’S NETWORK FOR DODOMA)

46. ELIMU MWANGAZA TANZANIA

47. EMPOWER SOCIETY, TRANSFORM LIVES (ESTL)

48. EQUALITY FOR GROWTH

49. FADHIL TEENS TANZANIA

50. FAIDIKA WOTE PAMOJA (FAWOPA)

51. FICOFAWE WOMEN FOUNDATION

52. GEITA PARALEGAL ORGANIZATION

53. GIRLS AND WOMEN WITH DISABILITIES DEVELOPMENT FOUNDATION

54. GIRLS EDUCATION SUPPORT INITIATIVES

55. GOSPEL COMMUNICATION NETWORK OF TANZANIA

56. HAKI CATALYST

57. HAKI ELIMU

58. HAKI MADINI

59. HAKI ZETU TANZANIA ORGANIZATION

60. HAPPY CHILDREN TANZANIA ORGANISATION

61. HUMAN RIGHTS NATIONAL ASSOCIATION OF EDUCATORS FOR WORLD PEACE

62. HUMANITY AID FOR DEVELOPMENT ORGANISATION

63. HURUMA ORGANIZATION

64. ILKISONGA PASTORALIST INITIATIVES (IPI)

65. INITIATIVE FOR GOOD GOVERNANCE AND TRANSPARENCE IN TANZANIA (IGT)

66. IRINGA PRESS CLUB

67. JAMBIAN MARINE AND BEACH CONSERVATION

68. JUKWAA LA KATIBA

69. JUMABECO

70. JUMAVIWACHA

71. JUMUIYA YA KUELIMISHA ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA UKIMWI NA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO (JUKAMKUM)

72. JUMUIYA YA KUENDELEZA UFUGAJI NYUKI NA UHIFADHI MAZINGIRA (JUKUNUM)

73. JUMUIYA YA KULINDA NA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO MKOANI (JUKUWAM)

74. JUMUIYA YA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO SHRHIYA YA OLE (JUKUHAWA)

75. JUMUIYA YA MAENDELEO YA ELIMU KWA WATOTO PEMBA (JUMAEWAPE)

76. JUMUIYA YA MAENDELEO YA ELIMU KWA WATOTO PEMBA (JUMAEWAPE)

77. JUMUIYA YA MAENDELEO YA WAVUVI WA KOJANI (KOFDO)

78. JUMUIYA YA MAENDELEO ZIWANI (JUMAJZI)

79. JUMUIYA YA OWEDE

80. JUMUIYA YA TUMAINI JIPYA PEMBA(TUJIPE)

81. JUMUIYA YA TUSISHINDWE DEVELOPMENT ORGANISATION PEMBA (TUDOPE)

82. JUMUIYA YA WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA (JUWASPE)

83. KAGERA HUMAN RIGHTS DEFENDERS & LEGAL AID SUPPORT ORGANIZATION

84. KIGOMA PARALEGAL AID CENTRE(KIPACE)

85. KIGOMA WOMEN DEVELOPMENT

86. KIKUNDI CHA SAWABI

87. KIKUNDI CHA USHINDI

88. KIOTA WOMENS HEALTH AND DEVELOPMENT (KIWOHEDE)

89. KOK FOUNDATION

90. KONGA BIHARAMULO

91. LARETOK-LE-SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU NGORONGORO (LASHEHABINGO)

92. Legal and Human Rights Centre (LHRC)

93. LINDI REGIONAL PRESS CLUB (LRPC)

94. LINDI WOMEN PARALEGAL AID CENTRE (LIWOPAC)

95. LIWALE FARMERS ASSOCIATION (LIFA)

96. MAASAI PASTORALIST DEVELOPMENT ORGANIZATION(MPDO-LARETO)

97. MAGATA PRIMARY COOPERATIVE SOCIETY

98. MANYARA REGIONAL CIVIL SOCIETY NETWORK (MACSNET)

99. MBEYA PARALEGAL AID CENTRE (MBEPACE)

100. MBEYA WOMEN

101. MCHOMORO AIDS COMBAT GROUP

102. MEDIA ASSOCIATION FOR INDIGENOUS AND PASTORALIST COMMUNITIES

103. MEDIASPACE TANZANIA

104. MICHEWENI ISLAMIC DEVELOPMENT ENVIRONMENTAL CONSERVATION AND AIDS CONTROL (MIDECAC)

105. MIKONO YETU CENTRE FOR CREATIVITY AND INNOVATION (MIKONO YETU)

106. MOROGORO PARALEGAL CENTRE (MPLC)

107. MSICHANA INITIATIVES

108. MTWARA NGOS NETWORK(MTWANGONET)

109. MTWARA PARALEGAL CENTRE

110. MTWARA YOUTH ANTI AIDS GROUP

111. MUKEMBA GROUP MAENDELEO

112. MWANZA PRESS CLUB

113. NAMNYAKI MAASAI GIRLS AND WOMEN ORGANIZATION (NAMGWO)

114. NATIONAL UNION OF MINE AND ENERGY WORKERS OF TANZANIA (NUMET )

115. NEW HOPE NEW WINNERS FOUNDATION (NHNWF)

116. NGUVUMALI COMMUNITY DEVELOPMENT OF ENVIRONMENT

117. NOMADIC PASTORALIST DEVELOPMENT ORGANIZATION (NOPADEO)

118. NYAKITONTO YOUTH FOR DEVELOPMENT TANZANIA (NYDT)

119. OPEN MIND TANZANIA

120. ORGANISATION FOR RURAL SELF-HELP INITIATIVES (ORSHI)

121. PAMOJA DAIMA (PADA)

122. PARALEGAL PRIMARY JUSTICE (PPJ)

123. PEACE RELIEF ORGANISATION (PRO)

124. PEMBA ASSOCIATION FOR CIVIL SOCIETY ORGANISATION (PASCO)

125. PEMBA EAST ZONE ENVIROMENT ASSOCIATION (PEZEA)

126. PEMBA ENVIRONMENT AND MALARIA CONTROL (PEMCO)

127. PEMBA ISLAND RELIEF ORGANIZATION (PIRO)

128. PEOPLES DEVELOPMENT FORUM (PDF)

129. PEOPLES HEALTH MOVEMENT TANZANIA (PHM)

130. PINGOS FORUM

131. POVERTY ALLEVATION IN TANGA (POVATA)

132. PROMOTION AND WOMEN DEVELOPMENT ASSOCIATION(POWDA)

133. PROSPEROUS HEALTH LIFE INITIATIVES (PHLI)

134. RAFIKI SOCIAL DEVELOPMENT ORGANIZATION

135. RESOURCE ADVOCACY INIATIATVE (RAI)

136. ROWODO

137. RUANGWA ORGANISATION FOR POVERTY ALLAEVIATION (ROPA)

138. RUJEWA INTERGRATED EFFORTS TO FIGHT POVERTY (RIEFP)

139. RURAL WOMAN DEVELOPMENT INITIATIVE (RUWODI)

140. SADELINE HEALTH CARE TRUST

141. SAFE SPACE FOR CHILDREN AND YOUTH WOMEN TANZANIA (SSCYWT)

142. SAKALE DEVELOPMENT FOUNDATION

143. SAUTI YA HAKI TANZANIA

144. SAUTI YA WANAWAKE UKEREWE

145. SAVE THE MOTHER AND CHILDREN OF CENTRAL TANZANIA (SMCCT)

146. SERVICE HEALTH AND DEVELOPMENT FOR PEOPLE

147. SHIRIKA LA BINADAMU NANDANGALA (SHIHABINA)

148. SIKIKA

149. SOUTHERN AFRICA HUMAN RIGHTS NGOS NETWORK (SAHRINGON)

150. SPORTS DEVELOPMENT AID LINDI

151. TANGA PARALEGAL AID

152. TANGIBLE INIATIVES FOR LOCAL DEVELOPMENT TANZANIA

153. TANZANIA AGRICULTURE MODERNIZATION

154. TANZANIA CENTRE FOR RESERCH AND INFORMATION ON PASTORALISM (TCRIP)

155. TANZANIA HOME ECONOMIC ASSOCIATION (TAHEA) BIHARAMULO

156. TANZANIA HUMAN RIGHTS DEFENDERS COALITION (THRDC)

157. TANZANIA INTERNATIONAL FELLLOWSHIP PORGRAMME ASSOCIATION (TIFPA)

158. TANZANIA LEGAL KNOWLEDGE AND AID CENTRE

159. TANZANIA MEDIA WOMANS ASSOCIATION (TAMWA)

160. TANZANIA MEDIA WOMEN’S ASSOCIATION-ZANZIBAR

161. TANZANIA NATURAL RESOURCE FORUM (TNRF)

162. TANZANIA NETWORK OF LEGAL PROVIDERS (TANLAP)

163. TANZANIA NETWORK OF WOMEN LIVING WITH HIV AND AIDS (TNW+)

164. TANZANIA PASTORALIST COMMUNITY FORUM (TPCF)

165. TANZANIA PEACE LEGAL AID JUSTICE

166. TANZANIA WIDOWS ASSOCIATION (TAWIA)

167. TANZANIA WOMEN EMPOWERMENT IN ACTION (TAWEA)

168. TANZANIA WOMEN LAWYERS ASSOCIATION (TAWLA)

169. TANZANIA YOUTH POTENTIAL ASSOSIATION

170. TGNP MTANDAO

171. THE AFRICAN FOR CIVIL SOCIETY(TACS)

172. THE AFRICAN INSTITUTE FOR COMPARATIVE AND INTERNATIONAL LAW (AICIL)

173. THE FOUNDATION OF HUMAN HEALTH AND SOCIAL DEVELOPMENT (HUHESO)

174. THE LIFE HOOD CHILDREN AND DEVELOPMENT SOCIETY (LICHIDE)

175. THE ORGANISATION OF JOURNALISTS AGAINST DRUG ABUSE AND CRIMES IN TANZANIA (OJADACT)

176. THE VOICE OF DISABLED WOMEN IN TANZANIA(VODIWOTA)

177. THE VOICE OF MARGINALIZED COMMUNITY

178. TRANSFORMATIVE INTERGRATIVE BUILDOUT FOR ALL (TIBA)

179. TREE OF HOPE

180. TUNDURU PARALEGAL CENTRE (TUPACE)

181. TUSHIRIKI

182. UMOJA WA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI NA UELIMISHAJI RIKA MAGU (UVUUMA)

183. UMOJA WA WAWEZESHAJI KIOO

184. UNION OF TANZANIA PRESS CLUBS (UTPC)

185. UVINZA NGOS NETWORK (UNON)

186. VITAL PROJECTION LIMITED

187. VOLUNTEER FOR YOUTH IN HEALTH AND DEVELOPMENT (VOYOHEDE)

188. WADADA SOLUTIONS ON GENDER BASED VIOLENCE (WASOGEBAVO)

189. WAJIBU INSTITUTE OF ACCOUNTABILITY

190. WALIO KATIKA MAPAMBANO NA AIDS TANZANIA(WAMATA)

191. WETE ENVIRONMENT CONSERVATION CLUB (WECOC)

192. WIDOWS AND ORPHANED DEVELOPMENT ORGANIZATION (WODEO)

193. WOMEN ACTION TOWARDS ENTRP.DEVELOPMENT

194. WOMEN LEGAL AID CENTRE (WLAC)

195. WOMEN WAKE-UP (WOWAP)

196. WOMEN’S PROMOTION CENTRE (WPC)

197. WOTE INITIATIVE FOR DEVELOPMENT EMPOWERMENT (WIDE)

198. WOTE SAWA YOUTH DOMESTIC WORKERS

199. YOUTH AGAINST AIDS POVERTY

200. ZANZIBAR AIDS ASSOCIATION AND SUPPORT FOR OPHARNS (ZASO)

201. ZANZIBAR ASSICIATION FOR CHILDREN ADVANCEMENT (ZACA)

202. ZANZIBAR CHILDREN RIGHTS FORUM

203. ZANZIBAR FEMALE LAWYERS ASSOCIATION (ZAFELA)

204. ZANZIBAR FIGHTING AGAINST YOUTH CHALLENGES ORGANIZATION (ZAFAYCO)

205. ZANZIBAR LEGAL SERVICE CENTRE (ZLSC)

206. ZANZIBAR ORGANIZATION FOR WOMEN AND CHILDREN HEALTH CARE SUPPORT (ZOWCHCS)

207. ZANZIBAR YOUTH FORUM