Jamii za wafugaji na wakusanya Matunda ni Jamii zenye utegemezi wa uoto wa asili kwa ajili ya kuishi kwao. Jamii hizi zina mahitaji mengi linapokuja suala la Ardhi na matumizi ya rasilimali za asili – kukosa kwao uwakilishi kwenye vyombo vya maamuzi ni chanzo kimojawapo cha kupelekea migogoro kadha wa kadha, hivyo ni vema zikapewa hamasa na kipaumbele kwenye kugombea ili kuhakikisha kwamba mahitaji yao yanajulikana na kufanyiwa kazi kikamilifu.
Kufuatia hilo, PINGO’s Forum imeandaa kijitabu hiki kipate kuwasaidia katika safari ya kugombea na kushika uongozi kwa ajili ya manufaa ya Jamii zao. Hata hivyo kijitabu hiki si tu kwamba kina manufaa kwa Jamii hizo tu, bali pia kwa mtu yeyote yule ambaye anaonyesha nia ya kuongoza jamii kwenye ngazi yoyote ile ama kwa sehemu kumtathmini kiongozi ama mtarajiwa.