Ardhi ndio msingi wa uzalishaji mali kwenye taifa lolote lile duniani. Hakuna shaka kwamba jamii zote zinauhitaji wa raslimali hii kwa matumizi mbalimbali. Hii huusish
a mipango ya matumizi bora ya ardhi ambapo maeneo ya makazi, maeneo ya malisho, maeneo ya hifadhi ya mazingira na maeneo ya makazi miongoni mwao hutengwa kulingana na sheria zinazotuongoza.
Ufuataji wa sheria na usimamizi wake kwa uthabiti huchangia jamii kuwa na amani ikiwemo uchache wa migogoro. Fuatilia kipindi hiki cha Morning Trumpet kama klivyorushwa na kituo cha Runinga cha Azam TV tarehe 14 Julai 2020 ambapo mwanasheria wa taasisi, Emanuel Saringe aliwakilisha akizungumzia nafasi ya Kijiji katika kusimamia ardhi na pia utoaji wa hatimiliki za kimila unavyochangia kupunguza migogoro ya ardhi.